Nyumba ya makazi ya mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia imeteketea kwa moto siku ya Jumamosi, majira ya saa saba u nusu mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa huenda ni hitilafu ya umeme unaosemekana kukatika asubuhi na kurejea mchana kwa nguvu kubwa.
Akizungumza
na Channel TEN, kaka wa Mbatia, Felix Kessy amesema hadi sasa
wanachoweza kueleza ni uharibifu uliotokea kutokana na moto huo, kwani
hawakuwepo wakati wa tukio, ingawa anawashukuru majirani walioweza
kuokoa baadhi ya vitu vya ndani.
Amesema
ni mapema mno kuzungumzia aina ya uharibifu kwani atakayeweza kujua
zaidi ni mkewe na Mbatia ambaye kwa wakati huo Channel TEN ilipofika,
haikuweza kuzungumza naye kwa sababu alikuwa amepandwa na shinikizo la
damu kutokana na tukio hilo.
Mkuu
wa oparesheni hiyo kutoka kikosi cha zima moto na uokoaji kwa wakati
huo nyumbani hapo sajenti Haji Madulika amesema kikosi chake kiliwahi
eneo la tukio ingawa kutokana na ukubwa wa moto, walishindwa kuokoa
baadhi ya vitu.
Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.
Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.