Meneja wa kampeni wa vyama vinavyounda umoja wa katiba(UKAWA) na waziri
mkuu mstaafu wa serikali ya CCM ya awamu ya tatu FREDERICK SUMAYE,
amewataka watanzania kupuuza tuhuma za ufisadi zilizotolewa na aliyekuwa
katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilborad Slaa dhidi ya mgombea urais wa UKAWA
Bw. Edward Lowassa pamoja na yeye na kueleza kwamba hawatapoteza muda
wa kumjibu kwani hizo ni hila zilizopangwa kutaka kufifisha mabadiliko
wanayohitaji kwa watanzania.
chanzo::East Africa Television