/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Hatimaye Rich Mavoko Afunguka Ya moyoni Kuhusu uhusiano wake na Diamond


Msanii wa muziki Bongo, Rich Mavoko amesema hana tatizo lolote na Diamond Platnumz licha ya kuondoka kwenye lebo ya WCB.

Muimbaji huyo kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema kilichotokea kati yake na lebo hiyo sio ugomvi bali ulifika mwisho wa biashara yao, hivyo sasa wapo vizuri pamoja na uongozi mzima wa lebo hiyo.

Katika hatua hatua nyingine Rich Mavoko amesema kuwa maneno yanayosikika mwanzoni kwenye video ya wimbo Ndegele hayawahusu WCB kwani walikuwa wanataka tu kuvuta attention ya mashabiki ila kuhusu kuwa ni diss kwa lebo sio kusudio lao kabisa.

Mwaka 2016 Rich Mavoko ndo alijiunga na WCB, wimbo wake wa kwanza kutoa chini ya lebo hiyo unakwenda kwa jina la Ibaki Stori, kisha Kokoro na nyinginezo, pia ameweza kufanya kazi na wasanii wengine nje ya WCB kama Fid Q, Stereo, Nay wa Mitego, Lulu Diva na wengine

Bonyeza Picha Hapo chini Kudownload App Ya Usiku wa Mahaba Uweze Kujiunga na Magroup ya WhatsApp Ya KIkubwa Utasoma Simulizi Tamu na Kujifunza Jinsi ya Kumridhisha Mpenzi wako Bonyeza Picha Chini au HAPA

KASI YA MAGUFULI YAIKUMBA CLOUDS FM, SOMA HAPA


Mkurugenzi wa Clouds Media Group ambao ni waandaaji wa tamasha la Fiesta, Ruge Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo halitakuwepo mwaka huu.

Amesema wameamua kuahirisha kufanya tamasha hilo mwaka huu kutokana na ufinyu wa muda uliobaki hasa baada ya kupisha kipindi cha uchaguzi.

“Tulijua tukimaliza kampeni tutafanya kwa mikoa michache lakini tumeona kwamba hakuna kitu kizuri kama kumsupport mheshimiwa Magufuli , hebu sasa hivi turudi kwanza tutulie tuache hii amsha amsha aliyoanza nayo ianze kufanya kazi tujipange kwaajili ya Fiesta 15 ambayo itafanyika mwaka kesho,” Ruge aliiambia XXL ya Clouds Fm.

“Tutakuwa tunafikisha miaka 15 ya Fiesta na nina uhakika itakuwa na ukubwa inayostahili kuliko kufanya kitu kidogo mwaka huu. Tumeona tuache mwaka kesho mikoa 15, miaka 15 ya Fiesta itakuwa kubwa zaidi. Hapa Kazi imebidi iivae Fiesta pia,” alisema.

Habari Mpya::Masha Na Mbunge Wa Chadema Wakamatwa Na polisi Mkoani Katavi.Habari Kamili ingia hapa

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence

Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha pamoja na viongozi wengine wa Chadema Wilaya ya Mpanda, wamekamatwa na polisi leo , kwa kile kinachodaiwa kufanya kampeni katika kambi ya wakimbizi ya Katumba, wilayani Mpanda bila kuwa na kibali maalum.

Masha ambaye alikihama chama cha CCM hivi karibuni na kujiunga na Chadema amezungumza na Mwananchi na kusema ameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Mpanda baada ya kufanya kampeni katika kambi hiyo.

Nilikwenda kufanya kampeni katika kambi hiyo ambayo ina wakimbizi ambao mimi mwenyewe niliwapa uraia mwaka 2009,"amesema Masha na kuongeza:
"Kampeni zinafanyika kule lakini kwa sababu wanazojua wao wametukamata wakati hao wanaoitwa wakimbizi niliwapa uraia kwa amri ya Rais.

Pamoja na Masha wengine waliokamatwa ni Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo, Gerald Kitabu, Abraham Mapunda, Mwenyekiti wa Chadema, Mpanda. Katibu wa Chadema jimbo la Nsimbo, Stanslaus Selemani, Dalas Damian, Lameck Constantine Momose na Francisco Sylvester .
Kwa mujibu wa Masha, polisi wamewachukua maelezo viongozi hao wa Chadema kuanzia saa 9 mchana na wameliza saa 10 jioni.
â€Å“Tulikamatwa kuanzia saa 7:15 mchana tukachukuliwa chini ya ulinzi mkali wa polisi toka Katumba hadi Mpanda mjini na kuanza kuhojiwa,” amesema.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Dhahiri Kidavashari amesema Masha amekamatwa leo saa 4 asubuhi akiwa na watu wengine sita kwa makosa ya kufanya mkutano bila kibali katika makazi ya wakimbizi.
Kamanda Kidavashari amesema viongozi hao wa Chadema walitumia uwanja wa kambi ya wakimbizi ya Kanoge na baadaye Katumba bila kuwa na kibali maalum baada ya kuona kuwa hakuna ratiba ya mkutano mwingine katika eneo hilo.

"Kufanya mkutano si tatizo, tatizo walifanya hivyo bila kibali, yale ni makazi ya wakimbizi wengine wamepewa uraia lakini wengine hawajapewa,"amesema Kidashari 

Sababu Za Rais Kikwete Kutovunja Baraza La Mawaziri Hadi Sasa Hizi Hapa=>


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ametoa mwongozo wa kisheria kufuatia sintofahamu iliyoibuka kwa baadhi ya watanzania kuhusu sababu zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutovunjwa kwa baraza la mawaziri hadi muda huu huku zikiwa zimebaki siku tano kufanya uchaguzi mkuu.

Masaju alieleza kuwa kisheria bado sio muda muafaka wa kuvunja baraza la mawaziri kwa kuwa waziri hupoteza sifa za kuwa waziri wa serikali ya Tanzania punde kabla ya rais mpya kupatikana.

“Mara tu kabla rais mteule hajashika madaraka hayo, ndipo waziri anapoteza nafasi yake ya kuwa waziri. Kwahiyo sasa hata uchaguzi hatujafanya,” alisema.

Aliongeza kuwa suala la siku chache zilizobaki bado liko kisheria kwa kuwa rais mpya bado hajapatikana.

“Japokuwa ni siku tano sasa zimebaki, lakini uchaguzi ukishafanyika na rais akapatikana, mara tu huyu rais mteule hajashika madaraka hayo ndipo waziri anapoteza sifa ya kuwa waziri,” aliongeza.

Majibu ya kisheria ya mwanasheria mkuu wa serikali yamekuja wakati ambapo taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vijiweni zikieleza kuwa huenda kutovunjwa kwa baraza la mawaziri kunacheleweshwa kwakuwa kuna hofu ya mawaziri wengi kukihama Chama Cha Mapinduzi.

Balozi Juma Mwapachu alikoleza tetesi hizo wakati alipokuwa akirudisha kadi ya Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za chama hicho zilizoko Mikocheni, Dar es Salaam baada ya kueleza kuwa uamuzi wake unaungwa mkono na mawaziri wengi wa serikali ya awamu ya nne.

Breaking News::: Aya Ndiyo Maamuzi Ya Mahakama Kuu Kuhusu Kesi Ya Kukaa Mita 200 Baada Ya Kupiga Kura Soma Hapa=>


Mahakama Kuu ya Tanzania, imehairisha kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo.

Jopo hilo la majaji linaloongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo pamoja na Lugano Mwandambo na Aloysius Mjujulizi limeahirisha kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mgombea ubunge Viti Maalum kupitia Chadema, Ammy Kibatala.

Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu walipokea notisi ya walalamikaji muda wa jioni hivyo hawakujiandaa.

“Mheshimiwa Jaji, tunaomba tupewe muda kwani tulipokea nyaraka hizi muda wa kazi ukiwa umekaribia kwisha hivyo hatukujiandaa, tunaomba tupewe muda kama ikiwezekana tulete majibu saa 8:30 Mchana leo kama mahakama itaona inapendeza,” alisema Wakili wa Serikali Obadia Kameya.

Kabla Majaji hawajatolea uamuzi ombi hilo walimshauri Wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala kubadilisha mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi wa Uchaguzi kwani ndiye mtendaji mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuangalia katiba Ibara ya 74, kifungu kidogo cha 7, inayosomeka “Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.”

Baada ya marekebisho hayo, kesi hiyo iliyovutia watu wengi iliahirishwa mpaka kesho saa 3

Mawakili upande wa mlalamikaji ni Peter Kibatala na Omary Msemwa, huku upande wa walalamikiwa ambayo ni Mwanasheria Mkuu na Tume ya Uchaguzi ni Obadia Kameya na Alecia Mbuya.

Katika kesi hiyo, mgombea huyo ambaye pia ni mpiga kura mwenye maslahi na uchaguzi mkuu ujao, ameomba mahakama kwa mujibu wa kifungu hicho sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ifafanue kuhusu haki za wapiga kura.

Mlalamikaji anaitaka mahakama iseme na kutafsiri kifungu hicho kinamaanisha nini kuhusu haki hiyo kufuatia kauli iliyotolewa na NEC pamoja na Rais Jakaya Kikwete kwamba wananchi wakishapiga kura hawaruhusiwi kukaa eneo la vituo vya kupigia kura umbali wa mita 200.

Aidha, anaitaka mahakama itamke kama ni halali kwa Rais na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuzuia wananchi kukaa kwa utulivu umbali huo ama la.

Lowassa: I am Prepared To Lead Nation As 5th President....


CHADEMA presidential candidate, Edward Lowassa has said he is well prepared and organised to lead the nation as the Union government's fifth president.

Lowassa  also promised Mbeya residents to provide free education from kindergarten to university levels with just 1.4trn/- in collected revenue.

He said the government has a lot of finances with several untapped revenue sources from natural resources.

Lowassa, who leads the rainbow coalition better known as Ukawa said last year's tax exemptions amounted to 1.6trn/- which could be enough to finance the country's education budget.

On employment the Chadema candidate who is supported by the Coalition of Peoples Constitution (Ukawa) said secondary school graduates will be deployed in the National Service whereby apart from patriotism the youths will be equipped with vocational skills.

He made the pledges when addressing the full-packed campaign rally held at Rwanda-Nzovwe grounds a few kilometers from Mbeya city centre.

Before the rally, Lowassa addressed similar rallies in Chunya and Mbarali districts.

He said the National Service capacity will be increased five times of the current size and capacity.  He said farmers will be enabled to practice modern agriculture as well as to sell their produce outside the country.

“I will form a common-man friendly government and establish a special bank for small scale entrepreneurs,” said Lowassa amid applause from the crowd.  He however pledged to improve health services and upgrade regional hospitals to referral hospitals.
Former prime minister Frederick Sumaye called upon residents to vote for the coalitions' candidate since the ruling party has failed to implement the promises it made to Tanzanians during the 2010 General Election.

He said the current government has failed to improve social services specifically education and health.

Sumaye, who was premier during the third phase period, noted that once voted into power, Lowassa will put a check on corruption and misuse of public funds as the two contribute to poor social services delivery. “Corruption is a critical problem ... Ukawa is determined and ready to control it for the betterment of Tanzanians,” Sumaye said.

Chadema National Chairman Freeman Mbowe said he has no trust with the National Electoral Commission (NEC).

He said Ukawa members will secure their votes by staying 200 meters from the polling stations.

According to Mbowe, the fifth government will be formed by Chadema because wananchi have already decided to opt for change.

He urged the police to implement their duties by adhering to work ethics and respect human rights before and after the elections.

“Elections mean your life ... we only has seven days to go, you should not make a mistake you must vote for Lowassa," Mbowe said.

Former CCM Chairman for Shinyanga Region, Khamis Mgeja urged the residents to weigh political parties by their election manifestos.

According to Mgeja, CCM promised better life to Tanzanians but todate millions of people live under extreme poverty.

He said Chadema will ensure better life for pastoralists, farmers, workers and other societal groups.

Former Home Affairs minister Lawrence Masha said they made a brave decision to cross to Chadema. He insisted on the electorate to observe the country’s laws during the elections.

Long time politician Kingunge Ngombale-Mwiru said the ruling party is about to split due to violation of its own constitution.

He said CCM can longer rule the nation calling on the residents to vote for Chadema.

“Chadema is very strong and determined to bring about change in the country... every citizen supports change,” said Ngombale-Mwiru, adding that he decided to leave the party even after serving it for 60 years.

CHADEMA WAZUNGUMZIA TUHUMA ZA MBOWE KUHAMISHA MABILIONI NJE YA NCHI, SOMA HAPA

.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekashangwazwa na tuhuma za uongo zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe za kuhamisha fedha katika akaunti za nje.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alieleza kuwa hakuna sheria inayomkataza mtu kutofanya biashara na kuhamisha fedha zake binafsi.

Akitaja vyombo hivyo alisema kuwa ni Magezeti ya Jambo Leo, Uhuru na Raia Tanzania ambayo alidai yana maslahi ya kisiasa kwani habari hiyo imeonekana kuhaririwa na mhariri mmoja kutokana na kutokuwa na uthibitisho wala ushahidi wa upande wa pili.

“Mimi ni mwandishi mwenzenu, naifahamu taaluma hii, ukisoma habari hiyo utaona inafanana kwa kila mstari, nukta hadi koma, inaelekea iliandikwa na mwandishi mmoja na kusambazwa kimaslahi kwa magazeti yote matatu na wahariri wakapachika” alisema Makene.

Alisema kuwa mwenyekiti huyo ni mfanyabiahara wa kimataifa ambaye anafanya biashara zake halali nje na ndani ya nchi zinazojulikana na serikali.Alisema magazeti hayo yanaandika ili kuwaondoa wananchi kwenye ajenda kubwa ya Uchaguzi sababu chama cha Mapinduzi kimeelemewa.

Jana Magazeti matatu yaliandika kuwa Freeman Mbowe, anatuhumiwa kuhongwa ili kumpitisha Edward Lowassa, kuwa mgombea urais wa chama hicho, yakimtuhumu kufanya uhamisho wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Uhuru, Jambo Leo na Raia Tanzania yaliandika kuwa zilikuwa ni njama za Mbowe, kufanya uamuzi wake wa kumpitisha Lowassa kuwania urais pasipo kushindanishwa na mtu ndani ya chama chake na ndani ya muda mfupi, uamuzi unaodaiwa kukigawa chama hicho,

Magazeti hayo kwa pamoja yaliandika kuwa Mbowe anahamisha hela hizo wakati wagombea kupitia chama chake hawana hela.

Hata hivyo Makene alifafanua kuwa hakuna sera ya Chadema kutumia pesa za mtu binafsi na biashara zake kwa ajili ya kusaidia wagombea, isipokuwa hela zinazopatikana kutokana na ruzuku hutumika kwa shughuli za chama na hesabu zake zinajulikana.

Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya Afunguka Haya Mengine Kuhusu Vifo Vinavyotokea na Nyota Za Lowassa Na Magufuli



Gladness Malya na Gabriel Ng’osha
DUH! Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya amesema vifo vya watu maarufu na wanasiasa bado vipo na vinasababishwa na mvutano mkali wa nyota za wagombea wawili wa urais, John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (Chadema)
Akizungumza na Ijumaa Wikienda alisema alishawahi kutabiri kutokea kwa matukio hayo tangu Desemba 28, 2014 na kusisitiza kuwa vifo hivyo bado vipo, watu maarufu watapotea na wanasiasa watafariki dunia.
“Nilitabiri tangu Desemba, 2014, kuwa wagombea watafariki dunia kwa sababu wagombea wawili wa Ukawa na CCM, kinajimu nyota zao zina mvutano mkubwa sana, herufi M inayosimama badala ya Magufuli, nyota yake ni ya samaki ambayo asili yake ni maji wakati herufi L kwa maana ya Lowassa, nyota yake ni mshale, ambayo kiasili ni moto na ndiyo maana uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ni wa matukio.”



Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya.

Akiendelea kusisitiza, alisema “Ndiyo maana hata kifo cha marehemu Filikunjombe na wenzake kimehusisha moto kwa maana ya helikopta ile kulipuka. Watu maarufu na wanasiasa wataendelea kupotea na kufariki dunia mpaka Uchaguzi Mkuu utakapoisha,” alisema Maalim Hassan.

Aidha mtabiri huyo amewataka Watanzania kukesha wakiomba ili kuepukana na matukio hayo sambamba na kuiombea amani nchi yetu ya Tanzania.

Ni takribani vifo 17 sasa vya wanasiasa walioiaga dunia katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, akiwemo Mwenyekiti Mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Emmanuel Makaidi, Mchungaji na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) Christopher Mtikila, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi) Celina Kombani, aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Lushoto (Chadema), Mohamed Mtoi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdalah Kigoda na wengine huku vifo vilitokea Ijumaa iliyopita kwa ajali ya helikopta ni vile vya watu wanne akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, Kapteni William Slaa (baba wa meya wa Ilala, Jerry Slaa) wengine ni Plasdua Haule na Egdi Francis.

Hii Ndio Sababu Kwanini UKAWA Wasitisha Kampeni Ngazi Zote soma Hapa


VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimesitisha kampeni zake ngazi zote ili kutoa fursa kwa wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mwenza, Dk. Emmanuel Makaidi.

Dk. Makaidi, aliyekuwa pia Mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD) alichokianzisha mwaka 1992, na mgombea ubunge jimbo la Masasi mkoani Mtwara, alifariki dunia Alhamisi wiki iliyopita katika hospitali ya Nyangao, Masasi, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).

Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene, akizungumza kwa niaba ya UKAWA, jana jijini Dar es Salaam, alisema usitishaji wa kampeni umelenga kuonesha heshima ya kipekee kwa Dk. Makaidi ambaye alijitoa muhanga katika kuimarisha UKAWA kwa hali na mali.

“Kesho (Leo) kuanzia saa tatu asubuhi tutakuwa viwanja vya Karimjee kwaajili ya kutoa heshima za mwisho kwa Dk. Makaidi, sambamba na hilo pia tutasitisha kampeni zetu za ngazi zote na katika shughuli hiyo viongozi wote wa kitaifa wa UKAWA pamoja mgombea Urais watakuwepo” alisema Makene.

Baada ya mwili wa Dk. Makaidi kuagwa katika viwanja vya Karimjee, shughuli ya mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 74 itahitimishwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Ratiba ya kampeni itaendelea Jumatano ya tarehe 21 Oktoba kwa mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa kwenda mkoani Morogoro kumalizia majimbo ambayo hakufika katika awamu yake ya kwanza ya kampeni mkoani hapo.

Majimbo hayo ni pamoja na jimbo la Kilombero, Mlimba, Mikumi, Ulanga Mashariki na Ulanga Magharibi.

Aya Ndio Mazoezi Ya Yanayofanywa Sasa Angalia Picha zaidi Hapa




Lowassa Atua Kwa Kishindo Tunduma Baada Ya Mitambo Kukorofisha Juzi..Tazama Picha Za Mafuriko Yake Hapa



Edward Ngoyai Lowassa na Mhe. Freeman Mbowe wakiongea na wanaanchi wa Tunduma,Jumatatu 19/10/2015 katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma
 
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwasili katika viwanja shule ya msingi Tunduma kwa ajili ya mkutano wa kampeni huku akiongozana na viongozi wengine wa CHADEMA na UKAWA,akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru,Jumatatu 19/10/2015

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mhe. Freeman Mbowe akiongea na wananchi wa Tunduma,Jumatatu 19/10/2015 katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma katika mjini wa Tunduma mkoani Mbeya

Taarifa Mpya Kuhusu Wanafunzi Wa Vyuo Wanaosafirishwa Kupiga Kura soma Hapa


Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kuwa kimejipanga kuhakikisha wananchi ambao sio wakazi wa maeneo husika mkoani humo hawashiriki kuwachagua viongozi wasiowahusu.

Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga aliyasema hayo hivi karibuni alipoongea na waandishi wa habari mkoani humo, ambapo alieleza kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliojiandikisha katika mkoa huo lakini hawaishi maeneo hayo hawataruhusiwa kupiga kura kuwachagua wabunge na madiwani.

“Zipo taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Ukawa wameanzisha utaratibu wa kukodi magari kwa ajili ya kuwaleta wanafunzi ambao wamejiandisha hapa kwa ajili ya kupiga kura. Huu ni ushahidi tosha kwamba sio wakazi wa Dodoma,” alisema Dunga.

“CCM tumejipanga kuhakikisha hawapigi kura za kiongozi asiyewahusu, mawakala wetu watakabidhiwa orodha ya wakazi na wataisimamia hiyo,” Dunga ananukuliwa.

Kulikuwepo na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna ‘wasamalia wema’ ambao wamejitolea kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura wakati wakiwa vyuoni na sasa wako majumbani, wanarudi katika maeneo waliyoandikishwa ili wapige kura. 
  
Kwa mujibu wa Dunga, huenda wanafunzi hao wakaambulia kupiga kura kumchagua rais pekee katika eneo walilojiandikishia walipokuwa wanasoma vyuoni hapo.

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI MPYA TENA... SOMA HAPA


RAIS Jakaya Kikwete amemteua Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayotajwa kuwa kubwa katika Afrika.

Akihutubia katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Massawe afuatilie barua yake rasmi ya uteuzi. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Februari mwaka huu, huku akitajwa kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini.

Kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam. Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.

Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamisi ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya kuboresha ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.

Mwishoni mwa Juni mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka, Zambia. Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao katika Bandari ya Dar es Salaam.

Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10, kutaongeza uwezo wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12 za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua 1,500

BREAKING NEWS::::YALIYOJILI MAHAKAMANI MORO HUKUMU YA SHEIKH PONDA...SOMA HAPA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro, leo imeahirisha kutoa hukumu katika kesi ya jinai Na.128/2013 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Hukumu hiyo imeahirishwa hadi Novemba 18, mwaka huu baada ya Hakimu Mkazi Mary Moyo aliyetarajiwa kutoa hukumu hiyo kuwa na matatizo ya kiafya.

Taarifa hiyo imeonekana kuwaudhi watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo la mahakama hiyo waliokuwa na shauku kubwa ya kujua hatima ya kiongozi huyo.

Hati ya mashitaka ya kesi ya Ponda ilikuwa na jumla ya mashitaka matatu lakini Julai 22 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mary Moyo alitoa uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu katika mashitaka mawili yaliyosalia .

Mkutano wa Kihistoria Wa LOWASSA jana Jijini Mbeya .....Ilikuwa ni Zaidi Ya Mafuriko


Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu", katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya Oktoba 18, 2015

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiongea na wananchi wa Mbeya mjini katika viwanja vya Rwanda-nzovwe jijini Mbeya jana Jumapili 18/10/2015,akiomba kura pamoja na kunadi sera zinazotekelezeka

Video::Mama Lowassa Atoa Kichapo Ukumbini baada ya Mlevi Kushika Sehemu Nyeti na Kumkosea adabu Angalia Hapa


Watu  wanatabia  Mbaya. Mama  wa  watu  kaingia  vizuri  ukumbukini, Njemba  ikamalamia  na  kumpapasa  sehemu  nyeti.

Uvumilivu  ukamshinda  mama Lowassa  na  kujibu  mapigo.

Video: Mama Regina  Lowassa  Beat a Guy Up After He Grabbed Her Buttyy

Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top