/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Hii Ndio Barua Ya Maalim Seif Sharif Hamad Aliyo Muandikia Papa Francis Kuhusu Mzozo wa Zazibar Soma Hapa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Francis kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake  kutishia watu wa upinzani,”ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan  wa Zanzibar  mwaka  1840  kibali cha  kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar  ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia  na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.

Wafanyabiashara Wapuuza Agizo la Siku 7 Lililotolewa na Rais Magufuli........ Kamanda Kova Atangaza Zawadi Nono Ya Mamilioni Kwa Atakayemdaka Mfanyabiashara Huyu


Makampuni 26 yamekaidi agizo la Rais John Magufuli lililowataka wafanyabiashara wote waliokwepa kodi kwenye Makontena 326 yaliobainika kupotea bandarini walipe kodi ndani siku saba.

Hata hivyo ni Makampuni 6  tu ndio yaliyotii agizo la Magufuli baada ya kulipa kodi iliyokadiliwakuwa  pamoja na faini.

Vilevile Makampuni 16 yamelipa kodi  nusu tu tofauti na ile iliyokadiliwa,ambapo  jana ndo ilikuwa siku ya mwisho toka siku aliyosema  Rais Magufuli kuwa ndani ya siku saba wawe wamelipa kodi hizo. Kodi iliyolipwa na makampuni haya 22 ni 
10,075,979,462.08

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mchana kwenye Makao ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla alisema  mpaka jana saa kumi jioni ni makampuni sita tu ndio yaliyolipa kodi hiyo huku mengine 16 yakilipa nusu ya madai ya kodi na Makampuni 26 yakishindwa kulipa kodi iliyotakiwa pamoja nafaini ya kukwepa kodi.
 
“Agizo la Rais Magufuli mwisho wake ni leo( jana) saa kumi jioni,lakini wafanyabiashara hao waliotorosha makontena yao  wamekaidi agizo hilo. Sisi TRA hatuna kingine cha kufanya, tunaiacha sheria ichukue mkondo wake,” alisema Bi Massala.
 
Bi Masalla aliwasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516..

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamisha Kova aliwaambia wanahabari kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi .

Kamishna Kova alidai kuwa anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo.
 
Alisema Mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu huyo (pichani)  atapewa zawadi nono ya milioni 20.

Alisema Jeshi la polisi pia linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. 
  
Kamanda Kova alisema uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

Alisema kati ya watuhumiwa hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na watumishi 03 wanatoka  Bandari kavu (ICD) YA AZAM  ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wanatuhmiwa  kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

Kamisha Kova alisema uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. 
  
Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati  makontena  2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014   kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.

Wafanyabiashara 21 watupwa rumande kwa kudharau usafi..Soma Zaidi Hapa


MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly amewaweka ndani wafanyabiashara 21 kwa saa 6 kwa kukiuka agizo la Rais la kufanya usafi na kufungua maduka kabla ya muda ulioelekezwa.

Mkuu huyo wa wilaya alichukua hatua hiyo juzi, baada ya wafanyabiashara hao kufungua maduka kabla ya saa nne Sikukuu ya Uhuru ya Desema 9, mwaka huu, huku wananchi wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mpwapwa na viunga vyake.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika viwanja vya Mnara wa Mashujaa, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuzingatia maagizo yatolewayo na viongozi wa Serikali kwa lengo la kuongeza ushirikiano zaidi.

Pia aliwataka kuendeleza utamaduni wa usafi kila baada ya wiki mbili na kuongeza kuwa watatunga sheria ndogo ya utunzaji wa mazingira katika mji wa Mpwapwa na viunga vyake.

Hata hivyo, wananchi walilalamikia halmashauri ya Mpwapwa kwa kushindwa kuweka vituo vya kukusanya taka na kusababisha wananchi kuvamia maeneo ya wazi na kutupa taka hovyo.

Alisema kukosekana kwa gari la usombaji taka katika mji wa Mpwapwa, ndio chanzo kikuu cha mji huo kuendelea kuwa mchafu. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Mohamed Maje alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya kukosa gari la kusomba taka.

Kuhusu vituo vya kukusanyia taka, aliamuru Ofisa Usafi na Mazingira wa halmashauri hiyo, Emanuel Sallo kukaa na wadau ili kuainisha maeneo hayo.

Kauli Ya TFF Kuhusu Nape Nnauye Kuteuliwa Kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo soma HAapa


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.

Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana.

Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.

Taarifa kwa Umma Kuhusu Mlipuko wa Homa ya Nguruwe Jijini Mwanza


Baada ya kuripotiwa ugonjwa wa Kipindupindu kutokea katika maeneo mbalimbali kanda ya Ziwa headlines zimerudi tena.
Uchunguzi uliofanywa na Maabara ya chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA umethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe katika Wilaya ya Nyamagana, Mwanza.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwanza, Yohana Sagenge amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ambao unasababishwa na Virusu aina ya African Swine fever Virus ambapo madhara yake ni makubwa na husababisha kifo kwa 100%. kwa wanyama hao.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi



Hii Ndio Listi Ya Marais Wanaongoza Kwa Kupendwa Afrika Unajua Magufuli Ni Wangapi Soma Hapa


Imethibitika katika uchunguzi uliofanya na taasisi moja inayojiushisha na tafiti mbalimbali imebainika kuwa rais wa Tanzania Mr. John Magufuli anaongoza katika bara la Afrika kuwa ni rais anaepedwa sana na raia wake kuliko rais yoyote barani humu.

Inasemekana rais huyu anakadiliwa na zaidi ya watu milion 35 ndani ya nchi yake pekee wanampenda toka moyoni kabisa , pia zaidi ya watu milion 4 mpaka 6 katika katika nchi za Kenya , na Uganda.

Pia imejumuisha na wale waishio nje ya bara hili, rais wa pili ni rais mpya wa Nigeria , Kagame kashika nafasi ya 3 akifatiwa na Zuma

KAULI ya Kwanza ya Mwigulu Nchemba Baada ya Kuteuliwa Kuwa Waziri na Rais Magufuli



Huu Ndio Ukweli Kuhusu Home Shopping Center Kuhusika Na Kukwepa Kodi Pamoja Na Kufilisika Soma Hapa


Baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao zikieleza kuwa kampuni ya Home Shopping Centre imefunga maduka yake kutokana na kukwepa kodi na kuhusika kwenye sakata la makontena yaliyopotea bandarini, uongozi wa kampuni hiyo umejitokeza na kupinga taarifa hizo.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imeeleza kuwa habari hizo sio za kweli na kueleza kuwa haijawahi kukwepa kodi na haihusiki kwa namna yoyote na makontena yaliyopotea bandarini.

“Home Shopping Centre Co. Limited haihusiki kabisa kwa njia yoyote ile na wizi, ukwepaji kodi, au potevu wa makontena 349 na yale zaidi ya 2431 yaliyoibuliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kamwe haijawahi kujihusisha na uhalifu huo wa kuiba makontena na kukwepa kodi,” ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mfilisi wa kampuni hiyo, Yusufu Mohamed.

Mohamed alieleza kuwa kampuni hiyo ilifunga maduka yake kama ambavyo makampuni mengine hufanya na sio vinginevyo.

Hivi Ndivyo Alhamisi inavyoakisi nyota ya Dk. Magufuli...Kuanzia Kuzaliwa Hadi Kushinda Urais Na Kuteuwa Baraza La Mawaziri Soma Hapa Zaidi Hapa


Kama ni suala la kusafiria nyota katika maisha, basi kwa Rais Dk. John Magufuli (pichani), Alhamisi ndiyo ya mafanikio zaidi kwake na amekuwa akiitumia katika matukio mbalimbali makubwa.

Kuzaliwa
Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ana miaka 56, alizaliwa Alhamisi Oktoba 29, 1959 Wilaya ya Chato mkoani Geita. Hiyo inamfanya kuwa siku muhimu sana kwake katika maisha.

Kushinda Urais
Alhamisi Oktoba 29, mwaka huu, wakati Dk. Magufuli akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilimtangaza rasmi kuwa mshindi wa nafasi ya urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Kuapishwa Urais
Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, Dk. Magufuli aliapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi Oktoba 29, mwaka huu.

Uteuzi wa mwanasheria mkuu
Baada ya kuapishwa Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, siku hiyo hiyo alitinga Ikulu kwa mara ya kwanza akiwa Rais na kumteua George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kumuapisha siku iliyofuata.

Uteuzi wa waziri mkuu
Alhamisi Novemba 19, mwaka huu, Dk. Magufuli alipeleka rasmi jina aliloliteua la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni na siku iliyofuata akamuapisha na kulizindua Bung

Naibu Mkurugenzi Takukuru
Alhamisi Desemba 3, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli, alimteua Valentino Mlowola, kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lilian Mashaka, aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Baraza la Mawaziri
Jana Alhamisi Desemba 10, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli alitangaza rasmi Baraza lake la Mawaziri ikiwa ni siku 42 tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa ujumla, matukio hayo yanaifanya siku ya Alhamisi kuzidi kuwa ya kipekee zaidi kwa Rais Dk. Magufuli kwani mbali ya kuonekana kuwa siku yake ya bahati, amekuwa akiitumia kufanya matukio makubwa ya kitaifa.

Breaking News: Rais Magufuli Atangaza Baraza Lake la Mawaziri Soma Hapa



Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakatibisha katika kikao hiki cha kutangaza baraza la mawaziri,
Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. 
Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
  
Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;
  
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Mawaziri; Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo
  
2. Mazingira: January Makamba, naibu Makamba
  
3. Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
  
4. Ulemavu: Waziri ni Anthonu Mavunde
  
5. Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi : Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu wake ni William Nash
  
6. Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
  
7. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
  
8. Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu bado
  
9. Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe
  
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan
  
11. Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi naibu bado
  
12. Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
  
13. Utalii: Waziri bado
  
14. Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
  
15. Sayansi na ufundi: Waziri bado, Naibu ni Stella Manyanya
  
16. Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
  
17. Wizara yaHabari l,Utamaduni na Wasanii : Waziri ni Nape Nnauye,
  
18. Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene

 ==>Habari kwa kina itawekwa hivi punde

Breaking News: Rais Magufuli Atangaza Baraza Lake la Mawaziri Soma Hapa


Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakatibisha katika kikao hiki cha kutangaza baraza la mawaziri,
Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. 
Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
  
Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;
  
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Mawaziri; Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo
  
2. Mazingira: January Makamba, naibu Makamba
  
3. Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
  
4. Ulemavu: Waziri ni Anthonu Mavunde
  
5. Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi : Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu wake ni William Nash
  
6. Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
  
7. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
  
8. Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu bado
  
9. Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe
  
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan
  
11. Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi naibu bado
  
12. Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
  
13. Utalii: Waziri bado
  
14. Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
  
15. Sayansi na ufundi: Waziri bado, Naibu ni Stella Manyanya
  
16. Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
  
17. Wizara yaHabari l,Utamaduni na Wasanii : Waziri ni Nape Nnauye,
  
18. Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene

 ==>Habari kwa kina itawekwa hivi punde

Kikwete Ajibu Tuhuma Za Kulea Ufisadi Bandarini, Awapiga Kijembe Ukawa


RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema katika uongozi wake wa miaka 10, hakuwahi kuagiza mtu asamehewe kontena lake lisilipe kodi na angefanya hivyo, mapato ya Serikali yasingeongezeka kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Akizungumza baada ya kuwashitukiza wananchi wa Chalinze katika soko kuu la eneo hilo kwa kuungana nao kufanya usafi kuitikia agizo la Rais John Magufuli jana asubuhi, Kikwete alisema katika uongozi wake hakuwahi kuagiza mtu anayestahili kulipa kodi asilipe kodi.

Alisema wakati huu ambao amepumzika baada ya kustaafu, amepata nafasi ya kusoma mitandao na magazeti mbalimbali na kukuta baadhi ya watu, wakimshutumu na kumtukana yeye na familia yake wakimhusisha na ukwepaji kodi.

“Ni afadhali wanishambulie mimi ila wamuache Rais Magufuli (John Pombe) afanye kazi, ni maneno ya walioshindwa wasinilaumu, aliyewashinda ni Magufuli sasa hawana la kusema. Ni sawa na siasa za maji taka, lakini watakuwa wanapoteza muda wao na kufanya kazi bure, kwa kuwa mimi sigombei kitu chochote tena.

“Wanahusisha mpaka na familia yangu, kama mimi mwenyewe sijawahi kuruhusu mtu hata mmoja atoe kontena bila kulipia kodi, siamini kama mke wangu (Mama Salma) au mwanangu Ridhiwani (Mbunge wa Chalinze), wangeweza kufanya hivyo tu na watu wakawasikiliza.

“Wanachonga tu, wengine wamesema Kikwete hachomoki, kwani nimechomeka nini?” Alihoji na kusababisha watu walioshirikiana naye kufanya usafi katika soko hilo kucheka na kuanza kushangilia.

Alisema nafasi ya urais aliyoaminiwa na Watanzania kwa miaka 10, ilikuwa yake na haikuwa na ubia na mkewe wala mtu mwingine yeyote.

Kikwete aliwataka Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli katika jitihada anazofanya za kukabiliana na wakwepa kodi, huku akitoa mfano akisema wakwepa kodi kwa Serikali ni kama inzi na kidonda, hawaondoki bila kufukuzwa na ukiacha kuwafukuza wanarudi.

“Serikali ina wajibu kwa wananchi, wanataka barabara, shule, hospitali ziwe na dawa na mengine mengi, lakini haya yote yanahitaji fedha na Serikali inapata fedha kutoka katika vyanzo vya kodi,” alisema.

Alisema pia yapo mapato mengine ikiwemo ushuru mbalimbali kama katika kulipia leseni, hati za kusafiria na nyingine, lakini pia Serikali inaweza kuchukua mikopo na misaada.

Kikwete alisisitiza kuwa wakati wa uongozi wake, kazi hiyo ya kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ilifanyika, ndio maana alifanikiwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Pamoja na mafanikio hayo ya uongozi wake, Kikwete alisema bado mahitaji ya Serikali kwa watu wake, yameendelea kuwa makubwa kuliko upatikanaji wa mapato.

“Tunapaswa kuendelea kuboresha mifumo ya kodi, taasisi za mapato na kupata watendaji waadilifu, kwa kuwa kama mifumo na taasisi vikiwa imara, lakini watendaji si waaminifu haisaidii.

Alisema kazi hiyo anayofanya Dk Magufuli ni kubwa kwa kuwa inahusisha kunyang’anya tonge watu na kusisistiza namna bora ya kumuunga mkono ni kulipa kodi na wakusanyaji wa mapato ya Serikali wawe waaminifu.

Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alisema hata katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho walichokaa juzi, waliamua kumuunga mkono Rais Magufuli na kuwataka wanachama wote wa chama hicho kufanya hivyo.

“Ni pale tu mapato yatakapoongezeka, ndipo wajibu wa Serikali katika kuhudumia wananchi utawezekana, tukimuunga mkono Rais wetu mzuri ataweza na mapato yakiongezeka, maji yatapatikana, mapato yakiongezeka, zahanati na hospitali zetu zitapata dawa za kutosha, mapato yakiongezeka barabara za lami zitajengwa,” alisisitiza.

Alisema katika Serikali Kuu, makusanyo yako nyuma ya asilimia 10 ya lengo, lakini kwa juhudi za Rais Magufuli, hali inavyokwenda lengo hilo litapitwa na Serikali itaanza kuzungumzia makusanyo ya matrilioni kwa mwezi.

Hata hivyo, alisema juhudi hizo za Serikali Kuu hazionekani katika halmashauri ambako ni kama hakuna kazi inayofanyika na hata pale kunapokuwa na juhudi za kukusanya mapato, wakati mwingine yanaishia mikononi mwa wajanja.

Kikwete ambaye alifanya usafi katika soko ikiwemo kufagia, kukusanya na kuzoa taka akiwa na mkewe, huku akikataa kuvaa vifaa vya kuzuia vumbi, aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi.

Alisema uamuzi wa Rais Magufuli wa kutumia maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru, kuwataka wananchi wote wafanye usafi, ni wa busara na si wa kukurupuka kwa kuwa mwaka huu taifa lilikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Kauli Ya Lowassa Kuhusu Magufuli Kutekeleza Hoja Zake Na ilani Ya Chadema Soma Hapa


Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni.

Lowassa aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu Saye) na mwanae.

“Haya mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema Lowassa.

Kauli hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo, majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.

CUF wazungumzia taarifa za kufariki Maalim Seif, watoa msimamo wao kuhusu Uchaguzi Zanzibar..Soma Hapa


Chama cha Wananchi (CUF) kimekanusha vikali taarifa zilizosambazwa na watu ambao hawajajulikana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki.
Akiongea na ITV, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Ismail Jusa amesema kuwa taarifa hizo zina lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi kwa kutengeneza taharuki.
Jusa ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa waliopika na kusambaza habari hizo kwa kuwa mbali na kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif ni Kiongozi wa ngazi za juu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar..
“Yeyote aliyekuwa nyuma ya kusambaza uvumi huu hakuwa na nia njema. Na utaona kama ina malengo ya kisiasa kwa sababu taarifa yenyewe imehusishwa kwamba eti tukio hilo limetokea baada ya kujaribu kuwashawishi wajumbe wa vikao vyake vya CUF eti wasaini waraka wa kutaka uchaguzi urudiwe, jambo ambalo halipo,” alisema Jusa.

Taarifa hizo za kugushi zilizosambaa ziliwekewa nembo ya mtandao wa Facebook wa ITV, hali iliyokilazimu kituo cha ITV kukanusha vikali kuhusika na taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Jusa alieleza kuwa msimamo wa CUF kuhusu uchaguzi wa Zanzibar uko wazi kuwa hakuna kurudia uchaguzi na kwamba mshindi ambaye wanaamini ni Maalim Seif atangazwe

Picha Hizi Za Wadada Wakifanya Usafi Siku Ya UHURU Zawa Gumzo Mtandaoni Jionee Mwenyewe Hapa




After Lots of Rumors Finally Quick Racka Confirms Dating Kajala


There have been lots of speculations and rumors about Kajala dating Bongo Flava singer Quick Racka. Media did write about their secret relationship although they both denied it. Even Quick Racka had tattoo of Kajala's name. But speaking with Clouds fm Quick Racka was asked wheather he is still with Kajala or have already parted ways the singer replied they are still together ...

"Sometimes some things have to stay private because when love life get in public all the time rumors spread all the time too so sometimes it is better to be private but we are doing good...words on the streets are lots but we are the ones who know the truth" said Quick Racka

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE NA MKEWE SALMA NAO WAA MUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KATIKA USAFI ANGALIA PICHA

Raisi wa Awamu ya 4 Mh Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete nao wapo kwenye maeneo yao hivi sasa wanafanya Usafi. #UhuruWaUsafi #UsafiDay

Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi...Angalia Picha Hapa..Kweli Uyu Ndio Kiongozi Wa Mfano Soma

Leo Rais John Magufuli ameongoza Watanzania kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi, yuko eneo la ufukwe karibia na Ikulu akifanya usafi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye yuko kwenye soko la Kariakoo akiongoza wafanyabiashara wa soko hilo kufanya usafi.

Embedded image permalink

Ni siku ya kihistoria kwa taifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwamba siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania watu huelekea viwanja vya Uhuru kuungana na wengine kuadhimisha siku hii ambapo leo ni miaka 54 tangu uhuru kupatikana,lakini  watu wanafanya usafi kuboresha mazingira ikielezwa ni UHURU na KAZI,ikienda sambamba na kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu

Salam za Rais Magufuli kwa Wananchi katika Kuadhimisha Miaka 54 ya Uhuru


Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeiwezesha nchi yetu kutimiza miaka 54 ya uhuru kwa salama na amani. 
 
Namshukuru Mungu pia kwa kuniwezesha kuiona siku hii nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 
Napenda kuchukua fursa hii, kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa Taifa letu kutimiza 54 ya Uhuru tarehe 09 Desemba, 2015.
 
Napenda kuwahakikishia kwamba, kama ilivyokuwa kwa Serikali za awamu zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano itafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba Uhuru, Amani na Umoja na wa Taifa letu hauchezewi na mtu, kikundi au Taifa lolote.
 
Tutaendelea kudumisha Uhuru wetu na Mapinduzi ya Zanzibar, tunu ambazo ni msingi wa Muungano wetu na Utanzania wetu.

Tofauti na ilivyozoeleka tumeamua mwaka huu kusherekea kumbukumbu hizi kwa kufanya kazi,. Wakati tunapata Uhuru Taifa letu lilikuwa likiongozwa na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI. 
 
Kauli hii ilikuwa na lengo la kuamusha moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwa Watanzania kwa kutambua kuwa uhuru wetu hautakuwa na maana kama hatutafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujenga Taifa linalojitegemea.
 
 Watanzania katika miaka ile waliitikia wito huo kwa kufanya kazi za kuwaongezea kipato na za kujitolea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo.
 
 Katika miaka ya hivi karibuni moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwetu umepungua sana. Kwa sababu hiyo, niliamua kutumia siku ya kumbukumbu za uhuru wetu mwaka huu kukumbushana na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya UHURU NA KAZI kwa kufanya kazi hususan ya usafi wa mazingira. Madhimisho ya Uhuru mwakani yatasherehekewa kama kawaida.

Nawapongeza viongozi wa Mikoa na Wilaya na wa Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyojitokeza katika kuhakikisha kuwa zoezi la usafi wa mazingira linafanikiwa.

Napenda kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaweka mifumo na taratibu thabiti zitakazowezesha usafi wa miji yetu kuwa endelevu. 
 
Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri waache visingizio, uwezo na mamlaka ya kuhakikisha kwamba usafi katika miji yao unadumishwa wanao. Uwezo wa utendaji wao utapimwa pia kutokana na hali ya usafi wa miji yao.

Naomba wananchi tushirikiane katika kuhakikisha kuwa nyumba na mazingira ya nyumba zetu yanakuwa safi na maji ya kunywa katika maeneo ambayo hayawekwi dawa yanachemshwa.
 
 Aidha, wananchi wajizuie kutupa taka ovyo na viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wahakikishe kwamba kila nyumba inakuwa na choo.
 
 Tutashinda vita dhidi ya maradhi kama kipindupindu ikiwa sote tutazingatia kanuni za afya. Kila mtu atimize wajibu wake.

Mwalimu alisema Uhuru na Kazi na mimi nasema Hapa Kazi Tu.
Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top