Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Lawrence Masha pamoja na viongozi wengine wa Chadema Wilaya ya
Mpanda, wamekamatwa na polisi leo , kwa kile kinachodaiwa kufanya
kampeni katika kambi ya wakimbizi ya Katumba, wilayani Mpanda bila kuwa
na kibali maalum.
Masha ambaye alikihama chama cha CCM
hivi karibuni na kujiunga na Chadema amezungumza na Mwananchi na kusema
ameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Mpanda baada ya kufanya
kampeni katika kambi hiyo.
Nilikwenda kufanya
kampeni katika kambi hiyo ambayo ina wakimbizi ambao mimi mwenyewe
niliwapa uraia mwaka 2009,"amesema Masha na kuongeza:
"Kampeni
zinafanyika kule lakini kwa sababu wanazojua wao wametukamata wakati
hao wanaoitwa wakimbizi niliwapa uraia kwa amri ya Rais.
Pamoja
na Masha wengine waliokamatwa ni Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo, Gerald
Kitabu, Abraham Mapunda, Mwenyekiti wa Chadema, Mpanda. Katibu wa
Chadema jimbo la Nsimbo, Stanslaus Selemani, Dalas Damian, Lameck
Constantine Momose na Francisco Sylvester .
Kwa mujibu wa Masha, polisi wamewachukua maelezo viongozi hao wa Chadema kuanzia saa 9 mchana na wameliza saa 10 jioni.
“Tulikamatwa
kuanzia saa 7:15 mchana tukachukuliwa chini ya ulinzi mkali wa polisi
toka Katumba hadi Mpanda mjini na kuanza kuhojiwa,†amesema.
Akizungumza
na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Dhahiri
Kidavashari amesema Masha amekamatwa leo saa 4 asubuhi akiwa na watu
wengine sita kwa makosa ya kufanya mkutano bila kibali katika makazi ya
wakimbizi.
Kamanda Kidavashari amesema viongozi hao wa
Chadema walitumia uwanja wa kambi ya wakimbizi ya Kanoge na baadaye
Katumba bila kuwa na kibali maalum baada ya kuona kuwa hakuna ratiba ya
mkutano mwingine katika eneo hilo.
"Kufanya mkutano
si tatizo, tatizo walifanya hivyo bila kibali, yale ni makazi ya
wakimbizi wengine wamepewa uraia lakini wengine hawajapewa,"amesema
Kidashari