Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe amefariki dunia baada ya
helikopta aliyokuwa akiitumia kwaajili ya kampeni kupata ajali.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na meya wa manispaa ya Ilala,
Jerry Silaa ambaye pia amempoteza baba yake kwenye ajali hiyo.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya
uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na
rubani wamepoteza maisha," ameandika Silaa.
Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William
Silaa,nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa
pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani.
Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi," ameongeza.
"Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP
Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr.Meru, Kampuni ya Everest Aviation
,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga
wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine.รข€
Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo Capt.William Silaa akiwa na
Mhe. Deo Filikunjombe na abiria wengine walikuwa kwenye helikopta hiyo
yenye namba 5Y-DKK wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
Helikopta hiyo ilianguka kwenye msitu wa Selous.
"Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za
kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii,"Silaa aliandika kabla ya taarifa ya watu hao kupoteza maisha.