Mahakama
Kuu Dar leo imetupilia mbali shauri la tafsiri ya sheria ya mpigakura
kukaa au kutokaa umbali wa mitaa 200 kutoka eneo la kupiga kura.
Kwa
mujibu wa majaji waliotoa maamuzi hayo wamesema kuwa, kwa kuwa mikutano
ilishakatazwa kuwepo siku ya uchaguzi, hivyo hakuna mkutano, mkusanyiko
au vikundi vyovyote vitakavyoruhisiwa siku hiyo na kufanya hivyo ni
kuvunja sheria.
Pia wameeleza kuwa siku ya uchaguzi mtu yeyote atakayevaa sare ya chama chochote naye atakuwa amevunja sheria.
Kwa
upande wa wakili wa utetezi, Peter Kibatala amesema ameyapokea maamuzi
hayo lakini atakata rufaa juu ya shauri hilo kwa manufaa ya chaguzi
nyingine zijazo.