/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Alikiba aamsha mzuka wa mashabiki wake baada ya kutangaza ujio wa ngoma mpya


Msanii wa muziki, Alikiba ametangaza rasmi ujio wake mpya baada ya ukimya wa muda mrefu hasa hasa baada ya kujiingiza kwenye michezo.

Muimbaji huyo ametangaza kwamba ataachia wimbo ‘Hela’ hatua ambayo imeamsha hisia kwa mashabiki wake ambao walikuwa wanamsubiria kwa hamu.

Kiba ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya wadhamini wa timu ya Coastal Union kutoka Tanga inayoshiriki ligu Kuu ya soka Tanzania Bara (TPL), ameonekana kutumia muda wake mwingi kwenye soka kuliko kwenye muziki ambao umemtambulisha.

Mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii wameonekana kufurahishwa na kitendo hicho huku wengine wakitaka muimbaji huyo kuachia kazi hiyo mara moja.

Hata hivyo muimbaji huyo hajaweka wazi ni lini ataachia kazi hiyo inayosubiriwa kwa hamu ya mashabiki wa muziki.

Bonyeza Picha Hapo chini Kudownload App Ya Usiku wa Mahaba Uweze Kujiunga na Magroup ya WhatsApp Ya KIkubwa Utasoma Simulizi Tamu na Kujifunza Jinsi ya Kumridhisha Mpenzi wako Bonyeza Picha Chini au HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top