Laiti wana CHADEMA wangejenga utamaduni wa kuhoji kila uamuzi unaofanywa na viongozi wao, wakapinga au kukubali maamuzi hayo baada ya mijadala ya kina haya yasingetokea.
Kitendo cha CHADEMA kumkaribisha Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa kumechafua hali ya hewa ya kisiasa ndani ya chama.
Nakumbuka maneno aliyowahi kuyatamka Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dr Slaa kwamba kitendo cha CHADEMA kumleta Edward Lowassa ndani ya chama ni sawa na kuchota kinyesi na kukihamishia chumbani, hii haimaanishi kwamba Lowassa mwenyewe ni mchafu (fisadi) ila msururu wa marafiki zake wenye kashfa lukuki za ufisadi ndio wangekichafua chama.
Habari za kuibuliwa kwa tuhuma za watu walioshiriki katika kashfa ya fedha zilizoibiwa za Stanbick huku vinara wa skendo hizo wakiwa ni watu wa karibu wa Lowassa inazidi kuibua maswali mengi kuhusu uadilifu wa Eddo.
Mpende msipende wana CHADEMA kwa umoja wenu mmeamua kufanya uamuzi mbaya wa kukizika chama, CHADEMA wamepoteza mwelekeo,tangu wamlete Lowassa neno UFISADI limekuwa msamiati mchungu midomoni mwa CHADEMA, hawaongelei tena ufisadi.
Si Lowassa wala Mbowe aliyejitokeza kusifia jitihada za rais Magufuli katika kupambana na wahujumu uchumi nchini, si jambo la kustaahabu kutoka kwao kwasababu hata wakati wa kampeni hawakutaka kabisa kuongelea ufisadi.
Katika wakati huu ambao kashfa mbalimbali za ufisadi zinaibuliwa,wahusika wengi wanaotajwa ni watu wa Lowasaa na wengine walikuwepo katika timu ya kimkakati ya kampeni ya Lowassa.
Lile kundi la watu wenye kashfa lukuki za ufisadi sasa limehamia CHADEMA, bila kutarajia CHADEMA wamegeuka kuwa CCM ya miaka 2005 hadi 2015 ambapo ilikuwa ikiandamwa na ufisadi.
CHADEMA wamechukua kijiti sasa, sasa wajiandae kupokea mashambulizi makali kutoka kwa akina Nape bungeni, mkijaribu kuikosoa CCM watawakumbushia kuhusu Eddo na kundi lake mliowapokea huko CHADEMA.
Kwa kifupi,CHADEMA mmepoteza moral authority ya kuikosoa CCM kwa jambo lolote lile maana mmeamua kuyafanya yale yale mliyokuwa mkiwapigia kelele CCM.