Tutakachoshuhudia katika awamu hii ni kuibuliwa kwa madudu makubwa huku
wakuu wa mashirika ya umma wakiwajibishwa kama mbuzi wa kafara lakini
vigogo walioko kwenye system wakipeta au wakikamatwa wale dagaa tu.
Inawezekana kabisa,hawa wakuu wa mashirika haya ya umma walikuwa
wanafanya kazi tu ya kulinda maslahi ya wakubwa na huenda wao
wakawajibishwa huku vigogo hawa wakiachwa jambo ambalo serikali ya UKAWA
isingelifanya.
Kumekuwepo na madai/tuhuma za vigogo kutumia majina ya baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa kuendesha biashara zao kitu ambacho sidhani kama
serikali ya Magufuli itathubutu kukufanyia uchunguzi-UKAWA
wangethubutu.
Hivi biashara ya madawa ya kulevya, magogo,meno ya tembo na hata hii ya
kupitisha makontena kiholela bandarini haina baraka za wakubwa?Magufuli
ataweza kuwawajibishi vigogo hawa pindi wakibainika?
Fukuafukua hii ya serikali ya Magufuli huenda ikawa "counter-productive"
kwa CCM na serikali yake na jambo hili likiwa handled vibaya, huenda
likafanya watu waichukie zaidi CCM badala ya kuipenda kama wengi
wanavyodhani.
Anachokifanya hivi sasa Magufuli ni sawa kuwadhihirishia watanzani,tena
kwa ushahidi, ni kwanini CCM haikupaswa kuchaguliwa kurudi madarakani na
akishindwa kuwawajibisha vigogo watakaobainika atakuwa anajimaliza
mwenyewe.
Hivi sasa UKAWA wamerahisishiwa kazi kwani karibu kila kitu kinaibuliwa
na serikali yenyewe na wao kama wapinzani watakuwa na kazi ya
kushinikiza hatua zichukuliwe jambo ambalo nina mashaka kama
litatekelezwa kwa uaminifu hata kama itaundwa hiyo Mahakama ya Mafisadi.
Bungeni ndio kutakwenda kuchafuka na hapa ndio mtihani wa Magufuli na
serikali yake kuchukua hatua utakuwa mgumu zaidi maana ndani ya bunge
huenda yakaibuliwa mengi ambayo hatukuyatarajia.
Kwa mfano, yanayosemwa na watu na kuandikwa mitandaoni kuhusu kampuni ya
Home Shopping Center huenda yakaibukia Bungeni na wabunge wa UKAWA
wakadai uchunguzi ufanyike kuhusu kampuni hii.
Kufichua tuhuma na watuhumiwa ni jambo moja, na kushughulikia tuhuma na watuhumiwa ni jambo lingine.
Kwenye orodha hakuna wafadhili?