NA KENNETH NGELESI,MBEYA.
ALIYEKUWA mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kyela Mbeya,Abraham Mwanyamaki amefungua kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dr,Harrison Mwakyembe (CCM) katika mahakama kuu kanda ya Mbeya akidai yalikuwa na kasoro Lukuki.
Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye mahakama hiyo,Mwanyamaki alisema Dr, Mwakyembe hakushinda kihalali katika uchaguzi huo ambapo alipoona ameshindwa aliliamuru jeshi la polisi kuwatawanya watu kwa kuwapiga mabomu kisha kujitangazia ushindi kinyume na taratibu.
Alisema katika mchakato mzima kuanzia kura za maoni Mwakyembe alitoa Rushwa ya pesa na vitu kadhaa kwa wananchi akiwarubuni kumpa kurawakati wa uchaguzi ikiwemo kutoa kauli chafu katika kampeni na kuwa wakati wa majumuisho ya kuhesabu kura alimuamuru mkuu wa polisi kumpiga msimamizi wake.
Kwa upande wa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Clement Kasongo,alisema alikuwa na kila dariri za kuchakachua matokeo hayo baada ya kuingiza vituo hewa ambavyo havikuwepo kwenye orodha pomja na mambo mengine.
Mwanasheria aliyeishika kesi hiyo,Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya Advocates, Notaries Public Commissioners for oaths ya jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kuipitia nakuangalia kasoro hizo ameona kuna umuhimu wa kufungua kesi akiwa na matumaini ya kushinda kutokana na mazingira yenyewe.
Alisema mteja wake amefungua kesi ya kihistoria namba 2 ya mwaka 2015 akiwashitaki watu watatu ambao ni mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi Clement Kasongo, namba 2 ni Harrison Mwakyembe na watatu ni mwanasheria wa halmashauri kwa kukiuka taratibu za uchaguzi wakishirikiana kuchakachua matokeo.
Alisema endapo haki itatendeka anauhakika wa kushinda kesi hiyo na endapo haki haitatendeka watakata rufaa kwenye mahakama za juu kwa kuwa ushahidi wanao jinsi Dr,Mwakyembe alivyobumba ushindi huo akidaiwa kutumia cheo chake cha uwaziri kulitumikisha jeshi la polisi kuvunja kanuni za uchaguzi.
Wananchi kwa upande wao wakiongozwa na Merry Mwakipesile walisema wamesafiri kutoka wilayani kyela hadi mkoani Mbeya kuhakikisha kesi hiyo inafunguliwa ambapo alisema wao kama wananchi wanao ushahidi wa kutosha jinsi Mwakyembe na Tume walivyojipa ushindi huku wananchi wakipigwa na kuteswa.
Alisema kutokana na mazingira ya jimbo la Kyela wananchi walivyokuwa wakimzomea kila kona Dr,Mwakyembe baada ya kuwa mmoja kati ya wabunge mizigo nchini alivyolitelekeza jimbo hilo likiwa hoi,alijipanga kwa gharama kubwa ya kifedha kuhakikisha anashinda kwa nguvu.
Alisema licha ya kutumia kila njia ya kuhakikisha anashinda,lakini wao walimchagua mgombea wa chadema Abraham Mwanyamaki kwa kumpa kura za mtikisiko na kuwa cha ajabu wakashangaa wanapigwa mabomu bila sababu huku Mwakyembe akijitangaza mwenyewe kuwa ameshinda.
Debora Mwakipesile mkazi wa Kyela,alisema yeye ni mmoja wa wahanga walioteswa na kudharirishwa na jeshi la polisi na kuvunjwa mkono baada ya kukamatwa na kutiwa nguvuni huku baadhi ya askali wakimdharirisha kwa shinikizo la Mwakyembe.
Alisema kutokana na hali hiyo wao kama wananchi hawapo tayari kufanya kazi na Mwakyembe kwa kuwa sio chaguo lao ni chaguo la serikali na kuwa mbunge wao wanayemhitaji ni Abraham Mwanyamaki.
Aliye kuwa mgombea Ubunge jimbo la Kyela kwa tiketi ya chadema Abraham Mwanyamaki akiwa amembatana na Waikili wa kujitegemea kutoka kamapuni ya uwakili ya BM ya jijini Dar-es-salaam wakitoka nje ya mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya, mara baada ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge yaliyo mpa ushindi Dk Harison Mwakyembe wa chama caha mapinduzi
Wakili Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya BM ya jijijni Dar-es-salaam wa pili kushoto akitoka nje ya mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya mara baada ya kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Ubunge wa Dkt Harrison Mwakyembe wa CCM jimbo ya Kyela, wa pili kulia ni mlalamikaji katika kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2015,Abraham Mwanyamaki ambaye alikuwa mgombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema
Wakili wa kutitegemea kutoka kampuni ya binafsi ya Uwakili ya BM, Benjamin Mwakagamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, mara baada ya kufunguab kesi ya kupinga matokea ya UIbunge yaliyo mpa ushind Dk Harison Mwakyembe wa CCM,kulia ni kwake n I mteja nam mlalamika katkii keshi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 (Picha na Kenneth Ngelesi)