/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Lowassa awapa masharti Haya magumu polisi...Soma Zaidi Hapa

Aliyekuwa mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Marehemu Alphonce Mawazo jijini Mwanza leo

ALIYEKUWA mgombea Urais wa Chadema, Edward lowassa, amelitaka jeshi la Polisi nchini kuwachukulia hatua wale wote wanadaiwa kumuua, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo na kwamba kama hawatafanya hivyo, watachukua hatua wao wenyewe.
Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku mbili sasa tangu Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kutoa hukumu kwa chama hicho kikuu cha upinzani kumuaga na kumzika Marehemu Mawazo bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Marehemu Mawazo, alifariki Novemba 14 mwaka katika kijiji na kata ya Katoro, wilaya na Mkoa wa Geita na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Lowassa ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuaga mwili wa Mawazo kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amesema polisi wasipochukua hatua kwa waliomuua marehemu Mawazo watajichukulia hatua wao.
Amesema kuwa watu waliomuua Mawazo wanafahamika majina yao lakini Polisi kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuwachukulia hatua zozote zile mpaka sasa.
“Hawa Polisi wanafanya mambo yao kiimra-imra, kiujanja ujanja, wao wameleta magari ya washawasha yaliyonunuliwa kwa Dola za Kimarekani 282 milioni, hawana nama ya kuyatumia, wameamua kuwachokoza wananchi ili waweze kuyatumia.
“Wananchi nawaomba sisi tuache vurugu ili sasa hayo magari yao walionunua tuone watakavyo yatumia, wananua magari alafu shuleni hakuna madawati na barabara hakuna,” amesema Lowassa.
Pia amesema baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kutoa haki kwa familia na chama hicho kumuaga Mawazo, imeonekana jeshi la polisi halina intelejensia wanayodai bali ni waongo watupu.
Lowassa amesema hukumu ya Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, iwe somo kwa polisi wa Tanzania kutokana na kujawa wivu usiofahamika.
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akizungumza katika shughuli hiyo ya kuaga mwili huo, amesema haki imepatikana mahakamani na kuwaumbua polisi.
“Wananchi wamechoka kuuliwa kama ilivyotokea kwa wafuasi wa Chadema tangu mwaka 2011 mpaka sasa wakati huu wa Mawazo…tumechoka kufa, mwenye akili na afahamu,” amesema Mbowe.
Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya askari polisi wema na wenye kutekeleza weledi wa kazi zao kiufasaha, lakini wapo ambao hawafai kuwatumikia na kuwaongoza wananchi.
Aidha, aliwashukuru watu wote waliojitolea kuisaidia familia ya Marehemu Mawazo hasa mtoto wake Precious Mawazo (9) anayesoma darasa la nne akiwamo Lowassa pamoja na wabunge 113 wanaotoka vyama vya Ukawa, kwa kila mmoja kujitolea Sh. 300,000 na kupatikana 36 milioni.
Katika hatua nyingine, Mbowe amesema chama hicho kinajiandaa kumfungulia mashitaka ya madai Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, baada ya kuweka zuio la mwili wa Mawazo kutoagwa jijini Mwanza hadi Mahakama Kuu ilipotupilia mbali zuio hilo.
“Kamanada Mkumbo lazima alipe gharama zote za siku nane za kumweka Lowassa, Sumaye, Mbowe na wabunge zaidi ya 50 jijini Mwanza wakisubiri mahakama itende haki na hatimaye kushinda kesi,” amesema mwenyekiti Mbowe.

Newer Posts Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top