Baraza la vijana la chama cha Demokocrasia na maendeleo chadema BAVICHA wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA mkoani GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo hayatafanyika watalazimika kulipa kisasi.
Akizungumjza na wanahabari mchana wa leo jijini Dar es salaam katibu wa uenezi wa baraza hilo Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE amesema kuwa kwa sasa vijana na wanachama wa chadema wamechoka na mauaji ya viongozi wa chama hicho huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wahusika hivyo sasa wameamua kuhakikisha kuwa wanajilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wahusika wa tukio la Geita na kuwakamata kama polisi watakuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa muda muafaka..
Akizungumzia tukio la jana mkoani mwanza amesema kuwa wakati jana mwili wa marehemu MAWAZO ukiwasili katika hospitali ya BUGANDO kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa uchunguzi zaidi Polisi walipanga njama za kuutorosha mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuuzika kimya kimya jambo ambalo amesema wanachama na viongozi wa CHADEMA walishtuka na kuamua kulinda mwili huo na ndipo ilipotokea vurugu iliyopelekea kiongozi wa vijana taifa kukamatwa na polisi .
Amesema kuwa inashangaza kuona jeshi la polisi likiwa katika mstari wambele kuhangaika juu ya mwili wa Marehemu ALPHONCE MAWAZO wakati iko wazi kuwa wakati anauawa na wananchi polisi walikuwepo eneo la tukio na kushindwa kutoa hata msaada wa gari kwa ajili ya kumpeleka hospitalini lakini jana polisi walipata gari la kuja kumtorosha katika hospitali hiyo jambo ambalo amesema limekuwa likifanywa na polisi kila mara yanapotokea matukio ya mauaji kama haya.
Aidha katika hatua nyingine vijana hao wametangaza rasmi kuwa baada ya siku tatu na polisi kushindwa kuwaachia huru viongozi wao na kuwakamata wauaji wa MAWAZO wamewaagiza vijana wote wa Tanzania kukusanyika kwa wingi mkaoni mwanza kwa ajili ya kushinikiza kuwaachia viongozi wao pamoja na kulinda mwili wa marehemu ALPHONCE MAWAZO ambao umelazwa katika hospitali ya Bugando mkoani mwanza.
Marehemu ALPHONCE MAWAZO aliuawa na wananchi mkoani GEITA baada ya kushambuliwa na wananchi waliokuwa na sialaha za jadi ambao hadi sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleza hali halisi ya mauaji hayo.