Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dr. John Joseph Pombe Magufuli atangazwa rasmi kuwa mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2015 kutokana na idadi ya kura alizopata, Kadhalika mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan naye ametangazwa kuwa ameshinda uchaguzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Uchaguzi
Dkt. John Magufuli wa CCM ameshinda baada ya kupata
jumla ya kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 ya kura
zote halali na kumshinda mpinzani wake wa karibu,
Edward Ngoyayi Lowassa wa CHADEMA aliyepata kura
6,072,848 sawa na asilimia 39.97