/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Dk Slaa atimkia Marekani, nyumba italindwa na polisi.....Hapa Nimekuwekea Mazungumzo yake na Azam Tv Yaliyorushwa Leo Asubuhi


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa mapumziko.

Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwishandoka nchini kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.

Huku akiwa Marekani kupumzika na kujiendelea katika kozi fupi katika tasnia ya Sheria na Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo cha televisheni cha Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni Marekani, nyumba yake itakuwa inalindwa na Jeshi la Polisi kutokana na vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema.

“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa kupigwa mawe. Ni kweli ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha amesema anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika hoteli ya kifahari ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhoji wakati wa uchaguzi mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.

Kuhusu gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya Serena, Dk. Slaa amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama, alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za Chadema bali marafiki zake ambao hakuwaweka bayana.

Dk. Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa taifa, ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga kura muda ukifika.

Hapo  chini  Kuna Audio ya Mazungumzo  yaliyorushwa leo na Azam Tv wakati akihojiwas na Tido Mhando
Newer Posts Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top