Mh Mbowe amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, kitengo cha moyo, baada ya kuugua ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.
Nae
James Mbatia mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti
mwenza wa UKAWA, amefika hospitalini hapo kumjulia hali mh Mbowe, na
amesema pamoja na hali ya kuumwa ya mh Mbowe, wao bado wanaendelea
kufanya kazi na kwamba ratiba mbalimbali za vikao vya UKAWA ziko
palepale, na amewaomba watanzania kuwa watulivu na kuendelea kumuombea
mh Mbowe, apone haraka.