/* That's all, stop editing! Happy blogging. */

Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya Afunguka Haya Mengine Kuhusu Vifo Vinavyotokea na Nyota Za Lowassa Na Magufuli



Gladness Malya na Gabriel Ng’osha
DUH! Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya amesema vifo vya watu maarufu na wanasiasa bado vipo na vinasababishwa na mvutano mkali wa nyota za wagombea wawili wa urais, John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (Chadema)
Akizungumza na Ijumaa Wikienda alisema alishawahi kutabiri kutokea kwa matukio hayo tangu Desemba 28, 2014 na kusisitiza kuwa vifo hivyo bado vipo, watu maarufu watapotea na wanasiasa watafariki dunia.
“Nilitabiri tangu Desemba, 2014, kuwa wagombea watafariki dunia kwa sababu wagombea wawili wa Ukawa na CCM, kinajimu nyota zao zina mvutano mkubwa sana, herufi M inayosimama badala ya Magufuli, nyota yake ni ya samaki ambayo asili yake ni maji wakati herufi L kwa maana ya Lowassa, nyota yake ni mshale, ambayo kiasili ni moto na ndiyo maana uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ni wa matukio.”



Mtabiri bingwa na mtaalam wa nyota Afrika Mashariki, Maalim Hassan Yahya.

Akiendelea kusisitiza, alisema “Ndiyo maana hata kifo cha marehemu Filikunjombe na wenzake kimehusisha moto kwa maana ya helikopta ile kulipuka. Watu maarufu na wanasiasa wataendelea kupotea na kufariki dunia mpaka Uchaguzi Mkuu utakapoisha,” alisema Maalim Hassan.

Aidha mtabiri huyo amewataka Watanzania kukesha wakiomba ili kuepukana na matukio hayo sambamba na kuiombea amani nchi yetu ya Tanzania.

Ni takribani vifo 17 sasa vya wanasiasa walioiaga dunia katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, akiwemo Mwenyekiti Mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Emmanuel Makaidi, Mchungaji na Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) Christopher Mtikila, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi) Celina Kombani, aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Lushoto (Chadema), Mohamed Mtoi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdalah Kigoda na wengine huku vifo vilitokea Ijumaa iliyopita kwa ajali ya helikopta ni vile vya watu wanne akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, Kapteni William Slaa (baba wa meya wa Ilala, Jerry Slaa) wengine ni Plasdua Haule na Egdi Francis.
Newer Posts Older Posts
© Copyright BONGO CLASIC Published.. Blogger Templates
Back To Top