Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru na wahaki
Mwenyekiti  wa  ZEC  amewaambia  waandishi  wa  habari  mchana  huu  kuwa  amechukua  maamuzi  hayo  baada  ya  kujiridhisha  kuwa  uchaguzi  ulighubikwa  na  dosari  nyingi.
"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa....
"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"! - Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Sababu nyingine iliyochangia kufutwa kwa matokeo hayo ni pamoja na ikiukwaji wa sheria ikiwemo mgombea Maalim Seif kujitangaza kwenye matokeo kuwa mshindi.
Sababu nyingine iliyochangia kufutwa kwa matokeo hayo ni pamoja na ikiukwaji wa sheria ikiwemo mgombea Maalim Seif kujitangaza kwenye matokeo kuwa mshindi.